Napenda kumshukuru Mungu kwa zawadi ya maisha. Naamini Mungu
alikuwa na makusudi ya mimi kuwepo
katika hii dunia katika kizazi hiki na majira haya. Sifa na shukrani nampa
yeye.
Namshukuru Mungu kwa kuzaliwa kwangu na hata kunifanya mtu
niliyeko leo. Mungu amenipa neema yakuwa mikononi mwake na kunilinda mchana na
usiku kwa masaa yote Zaidi ya 227,760
sawa na miaka 26 niliyofanikiwa kuishi hapa duniani.
Kipekee sana namshukuru Mungu kwa ajili ya wazazi wangu (Grace
na Manase) pamoja na ndugu zangu wakike na wakiume (Elia, Eliaichi, Mage, Siah
na Elisante) kwa kunilea na kunitunza mpaka nimeweza kufika mahali naweza
kujitegemea mwenyewe, nawashukuru sana.
Kuna wakati niliugua, kuna wakati nilipata ajali, kuna
wakati nilikata tamaa, kuna wakati niliondokewa na ndugu zangu wa karibu, kuna
wakati nilifurahi na pia kuna wakati ambao yalinipitia mambo magumu na kuona kama
sina haja ya kuendelea kuishi tena lakini Mungu alinishika mkono na kuniongoza
vyema.
Mungu alinipa pia jamaa na marafiki wazuri walionitia moyo
na kuniunga mkono katika juhudi zangu za kupata mafanikio. Hakika sifa na
shukrani namrudishia Mungu aliye hai.
Nawashukuru sana marafiki zangu kwa msaada mkubwa wa mawazo, fedha, mali pamoja na kuwa mfano wa kuigwa kwangu uliochangia mimi kuwa mimi leo. Mungu awabariki sana, najua sitaweza kuwataja
wote maana ni wengi sana ila Mungu awabariki san sana.
Nawatakia kila la kheri katika maisha haya na yale yajayo.
Muzidi kubarikiwa
Na,
Godlove Materu
Copyright 2014 by Jennifer Kunst, PhD