Saturday 26 January 2019

ASANTE MUNGU NA MARAFIKI ZANGU, JANUARI 26 (KUKUMBUKA KUZALIWA)



Napenda kumshukuru Mungu kwa zawadi ya maisha. Naamini Mungu alikuwa  na makusudi ya mimi kuwepo katika hii dunia katika kizazi hiki na majira haya. Sifa na shukrani nampa yeye.
Namshukuru Mungu kwa kuzaliwa kwangu na hata kunifanya mtu niliyeko leo. Mungu amenipa neema yakuwa mikononi mwake na kunilinda mchana na usiku kwa masaa yote Zaidi ya  227,760 sawa na miaka 26 niliyofanikiwa kuishi hapa duniani.

Kipekee sana namshukuru Mungu kwa ajili ya wazazi wangu (Grace na Manase) pamoja na ndugu zangu wakike na wakiume (Elia, Eliaichi, Mage, Siah na Elisante) kwa kunilea na kunitunza mpaka nimeweza kufika mahali naweza kujitegemea mwenyewe, nawashukuru sana.
Kuna wakati niliugua, kuna wakati nilipata ajali, kuna wakati nilikata tamaa, kuna wakati niliondokewa na ndugu zangu wa karibu, kuna wakati nilifurahi na pia kuna wakati ambao yalinipitia mambo magumu na kuona kama sina haja ya kuendelea kuishi tena lakini Mungu alinishika mkono na kuniongoza vyema.

Mungu alinipa pia jamaa na marafiki wazuri walionitia moyo na kuniunga mkono katika juhudi zangu za kupata mafanikio. Hakika sifa na shukrani namrudishia Mungu aliye hai.

Nawashukuru sana marafiki zangu kwa msaada mkubwa wa mawazo, fedha, mali pamoja na kuwa mfano wa kuigwa kwangu uliochangia mimi kuwa mimi leo. Mungu awabariki sana, najua sitaweza kuwataja wote maana ni wengi sana ila Mungu awabariki san sana.
Nawatakia kila la kheri katika maisha haya na yale yajayo.
Muzidi kubarikiwa
Na,
Godlove Materu

0 maoni:

Post a Comment