SOMA
ninachoamini watu wote wanaotumia social media kama
hii, wana uwezo wa kusoma na kuandika kama wewe ulivyo.
hebu jaribu kusoma hapa inaweza ikakusaidia kwa namna moja
au nyingine!
umewahi kujiuliza, kuna utofauti gani kati ya maisha ya watu
walioishi zamani miaka hamsini iliyopita na sisi ambao tunaishi
leo?
nadhani utakubaliana na mimi kuwa watu wa kale walikuwa hawajui
mambo mengi kama ilivyo leo hii. leo watu wanafahamu mambo yao
pamoja na mambo ya wengine tena mbaaali kabisa. kwa mafano
unaweza ukawa unajua mila za kwenu na mila za kabila jingine kwa
kujifunza kupitia mtandaoni tuu.
Hii yote ni kwa ajili ya kukua kwa sayansí ya teknolojia mawasiliano
pamoja na uhuru wa vyombo vya habari.
Walahi tungejua matumiz mazur ya sayansi hii Kizazi cha leo
tungekuwa innovative kuliko hata akina newton, eistein na wengine
unaowafahamu.. lakini tumekuwa na matumiz mabaya ya mtandao
kwa kupotezeana muda kwa kushirikisha mambo yasiyo na maana
tukijisahau kuwa tuna wajibu wa kuandika historia za maisha yetu
kabla hatujafa.
Embu kijana funguka, ukiunga bando lako epuka suffing za vitu
visivyo na tija kwako. chukua vile vinavyokuhusu. kama ni mwanasiasa
fuatilia mambo ya siasa, mwanauchumi na uchumi, mwanateknolojia na
teknolojia, mwanahabari na habari za kujenga.
tuache kulike page zisizo na maana na zinazotufanya tusahau utu
wetu, epuka kushirikisha mambo yanayopotosha jamii na yanayojenga
upotevu wa amani.
TUMIA MTANDAO KWA KUJIFUNZIA, UTAONA FAIDA YAKE.
Asante kwa kusoma.
by Materu Godlove
information securty specialist
0 maoni:
Post a Comment