Monday 14 September 2015

CHANGAMOTO ZA MAISHA

CHANGAMOTO ZA MAISHA

Changamoto za misha zipo tokea enzi za mababu zetu. Hata changamoto tunazozipitia katika maisha yetu sasa si za kwanza wala hazitakuwa za mwisho pia. Kila mtu ana namna ya changamoto anazokumbana nazo. Ambazo zinaweza kuwa changamoto za

  • Uchumi kuyumba,
  • Ugonjwa au magonjwa,
  • Kukosa mtoto,
  • Kukataliwa na ndugu,
  • Kufeli mtihani
  • N.k
Hizo ni changamoto chache tuu ambazo nimeweza kuziorodhesha hapo. Kama una changamoto unayoipitia katika maisha yako, tambua kwamba wewe hautakuwa wa kwanza kukumbana nayo, nawala si wa mwisho kuipitia hiyo changamoto. Kwa maana hiyo basi, huna budi kujipa moyo na kusonga mbele, kwa kuamini kwamba utaishinda. Kamwe usikiri kusindwa, kwa maana anachokikiri mtu ndicho kinachomtokea katika masha yake. Ni lazima ujivike roho ya ushindi kwamba utaishinda changamoto yako. Ukitazama wapo watu waliopitia changamoto kama yako na wakashinda. Kwa nini wewe usishindwe?. Embu jivike imani dhabiti, hakika utashinda. Wapo watu waliougua UKIMWI wameombewa na Mungu amewapa uzima, wapo waliofeli shule lakini Mungu amewashindia katika maisha yao. Katika yote, tambua kuwa hata kama changamoto unayoipitia wewe yupo mtu ambaye aliwahi kuipitia katika maisha yake na akaishinda, njia aliyoipitia kushinda si lazima na wewe upitie hiyohiyo. Mungu anaweza kukupitisha njia tofauti kabisa kutatua changamoto yako. Hivyo usiache kumwomba Mungu ili akuonyeshe namna ya kuishinda changamoto unayokumbana nayo. Kitu kingine tambua kwamba kukata tamaa ni sumu ya mafanikio, na ukiwa mtu wa kukata tamaa, utashinwa kupokea muujiza wako. Unapaswa kujipa moyo na udhabiti wa imani katika kushinda changamoto unazopitia. Pia namna unavyokuwa mwepesi kumweleza rafiki yako juu ya changamoto zako, vivyo hivyo uwe mwepesi kumweleza Mungu changamoto unazokumbana nazo. Mungu ni zaidi hata ya huyo rafiki yako, rafiki yako ataishia kukupa moyo tuu, lakini Mungu atakupa faraja ya milele kwa kukuondolea kabisa tatizo lako. Kumbuka kuwa, Mungu anafahamu changamoto unazopitia hata kabla hujamwomba. Lakini unapofungua kinywa chako kumwomba atatenda kwa ajili yako. Mungu anasema Bisheni nanyi mtafunguliwa. Ubarikiwe sana rafiki yangu na Mungu akuonekanie katika changamoto unayapitia katika maisha yako. amen

0 maoni:

Post a Comment