hii ni picha ya kwanza

naweza nikaweka picha utakayo wewe.

Hii ni picha nyingine

nitaweka picha utakayo wewe.

Hii ni picha nyingine tena

Nitaweka picha upendayo wewe pia

Friday 27 November 2015

MATAJIRI WAKUBWA DUNIANI

It's good to have goals. If you're aiming to be among the top 10 richest people in the world, you might be interested in learning who you might have to displace. It can be instructive to review a list of the top 10 richest people in the world for other reasons, too, such as learning how they achieved their wealth and just how wealthy they are.
The top 10 richest people in the worldFirst off, here are the top 10:


Rank
Name
Net Worth
Source of Wealth
1
Bill Gates
$79.2 billion
Microsoft
2
Carlos Slim Helu & family
$77.1 billion
telecommunications
3
Warren Buffett
$72.7 billion
Berkshire Hathaway
4
Amancio Ortega
$64.5 billion
Zara
5
Larry Ellison
$54.3 billion
Oracle
6
Charles Koch
$42.9 billion
diversified
6
David Koch
$42.9 billion
diversified
8
Christy Walton & family
$41.7 billion
Wal-Mart
9
Jim Walton
$40.6 billion
Wal-Mart
10
Liliane Bettencourt & family
$40.1 billion
L'Oreal

Monday 14 September 2015

CHANGAMOTO ZA MAISHA

CHANGAMOTO ZA MAISHA

Changamoto za misha zipo tokea enzi za mababu zetu. Hata changamoto tunazozipitia katika maisha yetu sasa si za kwanza wala hazitakuwa za mwisho pia. Kila mtu ana namna ya changamoto anazokumbana nazo. Ambazo zinaweza kuwa changamoto za

  • Uchumi kuyumba,
  • Ugonjwa au magonjwa,
  • Kukosa mtoto,
  • Kukataliwa na ndugu,
  • Kufeli mtihani
  • N.k
Hizo ni changamoto chache tuu ambazo nimeweza kuziorodhesha hapo. Kama una changamoto unayoipitia katika maisha yako, tambua kwamba wewe hautakuwa wa kwanza kukumbana nayo, nawala si wa mwisho kuipitia hiyo changamoto. Kwa maana hiyo basi, huna budi kujipa moyo na kusonga mbele, kwa kuamini kwamba utaishinda. Kamwe usikiri kusindwa, kwa maana anachokikiri mtu ndicho kinachomtokea katika masha yake. Ni lazima ujivike roho ya ushindi kwamba utaishinda changamoto yako. Ukitazama wapo watu waliopitia changamoto kama yako na wakashinda. Kwa nini wewe usishindwe?. Embu jivike imani dhabiti, hakika utashinda. Wapo watu waliougua UKIMWI wameombewa na Mungu amewapa uzima, wapo waliofeli shule lakini Mungu amewashindia katika maisha yao. Katika yote, tambua kuwa hata kama changamoto unayoipitia wewe yupo mtu ambaye aliwahi kuipitia katika maisha yake na akaishinda, njia aliyoipitia kushinda si lazima na wewe upitie hiyohiyo. Mungu anaweza kukupitisha njia tofauti kabisa kutatua changamoto yako. Hivyo usiache kumwomba Mungu ili akuonyeshe namna ya kuishinda changamoto unayokumbana nayo. Kitu kingine tambua kwamba kukata tamaa ni sumu ya mafanikio, na ukiwa mtu wa kukata tamaa, utashinwa kupokea muujiza wako. Unapaswa kujipa moyo na udhabiti wa imani katika kushinda changamoto unazopitia. Pia namna unavyokuwa mwepesi kumweleza rafiki yako juu ya changamoto zako, vivyo hivyo uwe mwepesi kumweleza Mungu changamoto unazokumbana nazo. Mungu ni zaidi hata ya huyo rafiki yako, rafiki yako ataishia kukupa moyo tuu, lakini Mungu atakupa faraja ya milele kwa kukuondolea kabisa tatizo lako. Kumbuka kuwa, Mungu anafahamu changamoto unazopitia hata kabla hujamwomba. Lakini unapofungua kinywa chako kumwomba atatenda kwa ajili yako. Mungu anasema Bisheni nanyi mtafunguliwa. Ubarikiwe sana rafiki yangu na Mungu akuonekanie katika changamoto unayapitia katika maisha yako. amen

Thursday 3 September 2015

MSONGO WA MAWAZO

JINSI YA KUKABILIANA NA MSONGO WA MAWAZO,
Msongo wa mawazo ama stress kwa kiingereza, ni tatizo ambalo kwa bahati mbaya sana limeendelea kuwa kitu cha kawaida sana kwa wanaadamu katika zama tulizo nazo. Katika miaka hii tuliyo nayo, ni sahihi kabisa kusema kuwa, takriban wanaadamu wote walio hai wamekuwa wakikabiliwa na tatizo hili. Msongo wa mawazo unaweza kukufanya ushindwe kufanya shughuli zako za kila siku kwa ufanisi. Jambo la kufurahisha ni kuwa msongo wa mawazi unaepukika, leo nimechambua baadhi ya mambo ambayo yanaweza kukuwezesha kuepuka kupata msongo wa mawazo. Kuna baadhi ya aina za msongo wa kimawazo, ambazo zinaepukika na nyingine ni ngumu kuziepuka ila unapaswa kujua jinsi ya kukabiliana na shinikizo la msongo wa mawazo pale linapokukabili. MAMBO 5 YANAYOMKABILI MWANADAMU

  1. Kutojiamini
  2. Kuogopa mabadiliko
  3. Kukosa mpango wa maisha
  4. Kupuuza mahitaji muhimu ya binadamu ya:-
    • Mwili
    • Roho
    • Akili
  5. Kuishi kwa kukata tamaa
    • Kuumwa kichwa
    • Kukosa nguvu za mwili (me+ke)
    • Matatizo makubwa ya familia
    • Kukosa upendo
    • Hasira za mara kwa mara
      Waathirika wa msongo na kusambaratika Kila lika inakubwa na tatizo hili la Msongo wa Mawazo lakini nitajaribu kufafanua watu tofauti ambao hukubwa sana na tatizo hili

      Wazazi – sababu kubwa ni uchumi wa familia: Watoto wanaouwezo wa kukuhoji kwa nini wewe ni masikini, kushindwa kupeleka watoto shule, kushidwa kutatua matatizo hata madogo madogo ya Familia hapo lazima upate Msongo wa Mawazo

      Waajiri/Waajiriwa – Watu hawa hupatwa na tatizo hili na huwapelekea kuhamisha mambo ya kazini wanapeleka nyumbani na ya nyumbani wanayapeleka kazini. Mfano mtu amegobwana na wafanyakazi wenzake kwa makosa yake mwenyewe akarudi nyumbani na kuendelea na hali ile na kusababisha matatizo nyumbani kwake.

      Vijana na wanafunzi – Vijana wengi hukubwa na tatizo hili hasa katika maswala ya kiuchumi na kwa wanafunzi wengi kuingia katika Mapenzi wakiwa bado wapo shule huwasababishia msongo wa mawazo kwani tayari anakua kajipa majukum mengine. Mfano jana amegombana na mpenzi wake leo akienda shule hawezi kusoma vizuri atakua mtu mwenye mawazo kutokana na kilichomkuta siku iliyopita.

      Wanandoa – Wanandoa wengi wana msongo na kukosa faraja. Wanaamini nje kuna faraja zaidi (nyumba ndogo)

      Wakristo wanaweza kusoma vitabu hivi ili kupata maelezo (luka 24), (matendo 11:28-30), (yohana 18:14-27) Mizigo inayochosha

      Watu wengi hupata Msongo wa mawazo kutokana na wao kutaka kujitwika mizingo wasiyo weza kuibeba nitataja baadhi

      Kushindana na jirani
      Kufanya mambo nje ya uwezo wako
      Kupata bp, tumbo, kichwa, bila sababu
      Kuwa na idadi kubwa ya watoto ambao huwezi kuwalea
      Msongo wa mawazo hujitambulisha sana kwa mwili, akili na roho Akili – ikisikia juu ya jambo gumu inashindwa kulipokea. Inapeleka kwa tumbo, tumbo linashindwa linaamua kutoa unaharisha ndipo mtu hupata vidonda vya tumbo na tumbo kupata maumivu makali. Utakabiliana vipi na msongo
      1. Jifunze Kukubali Changamoto, Katika maisha huwa tunakutana na mambo ambayo hatukutaka kukutana nayo na pia tunashindwa kupata yale tuliyoyataka, karibu kila mtu huwa anapitia hali hii kwa namna moja au nyingine. Jifunze kukabili changamoto na sio kusikitika kwa nini mambo hayajawa kama ulivyotaka na kubaki ukisononeka. Jaribu kukubali mambo kwa busara zaidi, na utulivu huku ukitafakari nini cha kufanya ili kulipata lile ulilo kusudia. Changamoto iwe ni chachu ya wewe kuzidi kukazana na kujaribu zaidi.
      2. Jifunze kusema “hapana” hii ni katika mambo yako binafsi au kazi yako, unaitumiaje hii hapana? Unajua maofisini kuna swala la kupeana vikazi visivyoeleweka hata vimetokea wapi, yaani hujamaliza hili unaletea jingine hata kama sio kazi yako… sasa jifunze kukataa hizi kazi zisizo za kwako ili mradi tu mfurahishe tu. hivyo hivyo vitu vidogo vidogo ndivyo vinavyokuletea msongo wa mawazo.
      3. Jiepushe na watu ambao mara nyingi wanakusababishia Stress, Kunawakati huwa tunakua na kampani ya watu ambao kabisa unajua hawa wananisababishia msongo wa mawazo Mfano:- Upo katika mahusiano na mtu ambaye wewe unampenda lakini haonyeshi kujali upendo wako utajitahidi kupiga simu kutuma sms umweke karibu lakini yeye hajali, si busara ukaendelea kuumiza kichwa kwajili yake ni bora uachane nae mapema sana. Pia hata marafi wapo maadhi ya marafiki wanaweza wakakusababishia msongo wa mawazo kutokana na wanayokufanyia kwa mfano rafiki anayekupenda wakati wa raha tu na anakukimbia ukiwa na shida huyo si mwema kwako atakufanya uwe na Msongo wa mawazo. Tembelea watu wanaokufanya ufurahi na jifunze kucheka na kufurahi. Epuka kakaa na watu ambao kwako ni kikwazo.
      4. Panga kazi zako kwa ratiba usivuruge ratiba kwa vitu visivyo vya lazima ili kumfurahisha mtu mwingine. Mfano:- Umeapanga ratiba yako ya siku nzima anakuja rafiki ako akakuomba umsindikize sehemu ambayo haina umuhimu wala ulazima ukaenda ukapoteza mda mwingi huko, ukirudi tayari unakua umejipa Msongo kwani ratiba yako itakua imevurugika na utajilazimisha hata kuchelewa kulala ili tu umalize uliyo panga. Hiyo inaweza kukupa msongo kwani utakua ukifanya vitu kwa manung'uniko. katika ratiba yako tenganisha ratiba hiyo kwa vitu vya lazima kufanya na vitu vya kawaida ambavyo hata usipovifanya hazitakuharibia ratiba yako. kujua kipi cha lazima ni moja ya njia kubwa ya kupunguza msongo wa mawazo.
      5. Epuka Hasira za haraka, kuna mambo yanayohusu dini,siasa au maisha yako binafsi huwa yanakupa msongo wa mawazo basi jitahidi kuepukana nayo katika mazungumzo yako ya kila siku kwasababu yatakupa hasira na kukufanya ukasirike na hili hupelekea kuwa na msongo wa mawazo, ukiingia sehemu ukakuta watu wanaongelea swala hilo epuka kukaa nao karibu ili usiweze kuchangia na kujikuta unaingia katika mgogoro wa nafsi
      6. Fanya kazi yako ya halali kwa juhudi na maarifa
      7. Uwe na malengo ya maisha. Fanya jambo moja kwa wakati wake. Mfano jiulize unataka kufanya nini kwa wakati gani na ili uwe nani?
      8. Wakati unapokula usiwe unaonngea au kukumbuka shida zako. Pia kula polepole na kwa raha zako. Ikiwezekana wakati wa kula zima simu. kwasababu tunajua hatuwezi kuishi bila kula tujaribu kuheshimu mda wa kula kwani kunawakati hata simu zetu tunaweza kupokea kitu kikatufanya tuvuruge hata ratiba ya kula na kupoteza hamu na kusababisha Msongo wa mawazo.
      9. Fanya mazoezi kila siku, mara tano angalau kwa juma. Tofautisha kazi na mazoezi.
      10. Zingatia Muda wa kula
      11. Sikiliza muziki wa injili, bongo flava, lugha yenu ya asili, muziki ni dawa, nchi 2 za afrika ziliponya kwa muziki (Afrika kusini naKongo)
      12. Tafuta sababu zinazokuletea msongo wa mawazo, zitambue na kuzifahamu ili uziepuke.
      13. Usiweke Jambo Linalokusumbua Moyoni, Pale unapokutana na jambo ambalo umeshindwa kulitatua ni vyema ukamshirikisha mzazi wako au mlezi, rafiki wa karibu, mume au hata mshauri. Jifunze kutokuweka mambo yanayokuumiza moyoni maana katika hali hiyo ni rahisi sana kupata msongo wa mawazo. Uwe na tabia ya kupeleka wasiwasi na hofu zako zote mbele za Mungu kwa maombi na pia kuongea na mtu ambaye unajua atakuwa msaada kwako.
        1. NB: Msongo wa Mawazo si Ugonjwa na unaepukika ukijitahidi kufuata mambo hayo hautaweza kuwa na Msongo wa Mawazo. Jiamini kwa kila unachokofanya. Fikiri kabla ya kutenda, Kipende kila unachokifanya. Hapo utakua umeepuka msongo wa mawazo. Maamuzi yako ni bora kuliko yakuambiwa. Akili ya Kuambiwa Changanya na yako. asante kwa kusoma

USHAURI KWA NATUMIZI YA MTANDAO

SOMA

ninachoamini watu wote wanaotumia social media kama hii, wana uwezo wa kusoma na kuandika kama wewe ulivyo. hebu jaribu kusoma hapa inaweza ikakusaidia kwa namna moja au nyingine! umewahi kujiuliza, kuna utofauti gani kati ya maisha ya watu walioishi zamani miaka hamsini iliyopita na sisi ambao tunaishi leo? nadhani utakubaliana na mimi kuwa watu wa kale walikuwa hawajui mambo mengi kama ilivyo leo hii. leo watu wanafahamu mambo yao pamoja na mambo ya wengine tena mbaaali kabisa. kwa mafano unaweza ukawa unajua mila za kwenu na mila za kabila jingine kwa kujifunza kupitia mtandaoni tuu. Hii yote ni kwa ajili ya kukua kwa sayansí ya teknolojia mawasiliano pamoja na uhuru wa vyombo vya habari. Walahi tungejua matumiz mazur ya sayansi hii Kizazi cha leo tungekuwa innovative kuliko hata akina newton, eistein na wengine unaowafahamu.. lakini tumekuwa na matumiz mabaya ya mtandao kwa kupotezeana muda kwa kushirikisha mambo yasiyo na maana tukijisahau kuwa tuna wajibu wa kuandika historia za maisha yetu kabla hatujafa. Embu kijana funguka, ukiunga bando lako epuka suffing za vitu visivyo na tija kwako. chukua vile vinavyokuhusu. kama ni mwanasiasa fuatilia mambo ya siasa, mwanauchumi na uchumi, mwanateknolojia na teknolojia, mwanahabari na habari za kujenga. tuache kulike page zisizo na maana na zinazotufanya tusahau utu wetu, epuka kushirikisha mambo yanayopotosha jamii na yanayojenga upotevu wa amani. TUMIA MTANDAO KWA KUJIFUNZIA, UTAONA FAIDA YAKE.
Asante kwa kusoma.

by Materu Godlove


information securty specialist

Tuesday 6 January 2015

angalia uchekeke kidogo.

picha za godlove materu

picha za godlove materu


picha za godlove materu